Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU

SIKU YA KWANZA: IJUMAA KUU

KUHUSU HII NOVENA YA HURUMA YA MUNGU
Hizi ni sala ambazo Bwana Yesu mwenyewe alimfundisha Mtakatifu Sista Faustina Kowalska. Bwana Yesu alimwambia: “Kwa Novena hii, nitazijaza roho za watu kila neema iwezekanavyo. Uisali daima rozari hii niliyokufundisha. Na yeyote atakayeisali Rozari hii atajaliwa kupata Huruma Kuu ya Mungu saa ya kufa kwake, hata wakosefu shupavu wakisali Rozari hii, hata kama ni mara moja tu, wataipata Huruma Yangu isiyo na mwisho. Kwa njia ya Rozari hii, unaweza kuomba chochote na utakipata, bora tu kipatane na mapenzi yangu. Ninataka dunia nzima iijue Huruma Yangu isiyo na mwisho. Nami ninataka kuwapa neema nyingi wale wanaoitukuza Huruma Yangu, hata neema zile wasizofikiria kuzipata”. Kwa kila neno moja la Novena hii, tone moja la Damu Takatifu hutoka katika Moyo Mtakatifu wa Yesu na kuidondokea roho moja ya mkosefu.

“Heri mtu Yule ambaye katika maisha yake amejizoeza kuikimbilia Huruma ya Mungu, kwa maana siku ya Hukumu ya Mwisho hatahukumiwa. Huruma ya Mungu itamkinga. Mwanangu, wahimize watu waisali hii Rozari ya Huruma niliyokufundisha. Kwa kusali Rozari hii nitawapa kila neema watakayoniomba. Hata wakosefu wagumu wakiisali nitajaza roho zao kwa amani, na nitawajalia kifo chema. Wanapoisali Rozari hii karibu na mtu anayekufa, mimi nitasimama katikati ya roho hiyo na Baba Yangu, si kama Hakimu mwenye Haki, bali kama Mwokozi mwenye Huruma”.

NAMNA YA KUFANYA NOVENA KWA HURUMA YA MUNGU
Sala ya kutubu:
Mungu wangu, ninatubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi kwako, Amina.

Nia ya sala za leo:
SIKU YA KWANZA
Maneno ya Bwana Yesu: “Leo niletee wanadamu wote kijumla, hasa wakosefu wote. Uwazamishe ndani ya Bahari Kuu ya Huruma yangu. Kwa njia hii utatuliza uchungu wangu kwa ajili ya roho zilizopotea.”

Tuombe Huruma kwa ajili ya wanadamu wote, hasa kwa ajili ya wakosefu.
W. Ee Yesu mwenye Huruma kabisa, ambaye asili yako ni Huruma na Msamaha, usizitazame dhambi zetu, bali utazame tumaini tulilo nalo katika wema wako usio na mwisho. Utupokee sisi sote chini ya ulinzi wa Moyo wako wenye Huruma tele. Usimwache hata mmoja. Tunakuomba hayo kwa njia ya upendo ule unaokuunganisha wewe na Baba na Roho Mtakatifu, katika Umoja wa Utatu Mtakatifu, daima na milele. Amina.

Baba yetu …….. Salamu Maria ……... Atukuzwe …….…

W. Baba wa Milele, uwatazame kwa macho ya huruma wanadamu wote, na hasa wakosefu maskini, waliongizwa ndani ya Moyo wa Mwanao mpenzi, Bwana wetu Yesu Kristu, ulio na huruma yako kuu, ili nasi tuisifu na kuitukuza tangu sasa na milele yote. Amina.

Rozari  ya Huruma ya Mungu
(Tumia chembe za rozari ya kawaida)
Baba yetu …       Salamu Maria …. x3            Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi …….

Kwenye chembe kubwa
Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za dunia nzima.

kwenye chembe ndogo
Mwanzishaji: Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Wote huitika: Utuhurumie sisi na dunia nzima.

Mwisho wa Rozari sali mara tatu sala ifuatayo:
Mungu Mtakatifu, Mtakatifu mwenye Enzi, Mtakatifu unayeishi milele, Utuhurumie sisi na dunia nzima.


Litania ya Huruma ya Mungu

Post a Comment

0 Comments