NOVENA YA HURUMA YA MUNGU
SIKU YA SITA: JUMATANO BAADA YA PASAKA
NAMNA YA KUFANYA NOVENA KWA HURUMA YA MUNGU
Sala ya kutubu:
Mungu wangu, ninatubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi kwako, Amina.
Nia ya sala za leo:
SIKU YA SITA
Maneno ya Mwokozi wetu: “Leo niletee roho za watu walio wapole na wanyenyekevu wa moyo, pamoja na roho za watoto wadogo, na uzizamishe katika kilindi cha Huruma yangu. Roho hizi hufanana kwa ukaribu zaidi na Moyo wangu. Watu hawa ndio walionitia nguvu wakati wa mateso na uchungu wa mahututi yangu. Niliwaona kama malaika wa duniani, ambao watakesha daima kuabudu katika altare zangu. Kwa mafuriko yangu, nitawamwagia neema zangu zote, kwa maana ni roho ile tu iliyo na unyenyekevu inaweza kupata neema zangu. Ninawapendelea watu walio wanyenyekevu na kuwaamini sana.”
Tuwaombee watoto wadogo pamoja na roho zile zenye unyofu kama wao.
W. Ee Yesu mwenye Huruma sana, Wewe Mwenyewe ulisema: “Jifunzeni kwangu kwa maana Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa Moyo”, uwapokee ndani ya Moyo wako uliojaa Huruma, watu wote walio wapole na wanyenyekevu, pamoja na roho za watoto wadogo. Roho hizi hustaajabisha Mbingu nzima, maana wanapotokea mbele ya Kiti cha Enzi cha Baba wa mbinguni, huwa kama shada la maua litoalo harufu tamu ya marhamu safi, na kuifurahisha Mbingu nzima. Mungu Mwenyewe hufurahia manukato yao safi. Roho hizi zina makao ya daima ndani ya Moyo wako wenye Huruma ee Yesu. Na daima hukuimbia wimbo wa Huruma na Upendo wako. Amina.
Baba yetu …… Salamu Maria …….. Atukuzwe …….
W. Baba wa Milele, uzitazame kwa macho ya Huruma, roho za watu wote walio wapole na wanyenyekevu wa moyo, pamoja na roho za watoto wadogo, walioingizwa katika makao ambayo ni Moyo wa Yesu Mpenzi, ulio na Huruma nyingi. Roho za watu hawa, hufanana na Mwanao kwa kwa karibu zaidi. Harufu yao tamu ya fadhila hukufurahisha sana, nayo hupanda ikianzia hapa duniani mpaka kwenye Kiti chako Kitukufu. Ee Baba wa Huruma na wema wote, ninakuomba, kwa ule upendo ulio nao kwa roho hizi penzi, na kwa ajili ya furaha uipatayo kwao, utubariki sisi na dunia nzima, ili sote pamoja tuungane katika kuisifu Huruma Yako, kwa milele yote. Amina.
Rozari ya Huruma ya Mungu
(Tumia chembe za rozari ya kawaida)
Baba yetu … Salamu Maria …. x3 Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi …….
Kwenye chembe kubwa
Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za dunia nzima.
kwenye chembe ndogo
Mwanzishaji: Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Wote huitika: Utuhurumie sisi na dunia nzima.
Mwisho wa Rozari sali mara tatu sala ifuatayo:
Mungu Mtakatifu, Mtakatifu mwenye Enzi, Mtakatifu unayeishi milele, Utuhurumie sisi na dunia nzima.
Litania ya Huruma ya Mungu
0 Comments